Hukumu ya kuzipindisha maana sifa za Allaah

Swali: Anayetumbukia katika jambo la kupindisha maana sifa za Allaah ni katika mambo ya Ijtihaad?

Jibu: Hapana, hapana. Hili ni batili. Huo ni upotofu. Kitendo hicho ni miongoni mwa dini ya Jahmiyyah na Mu´tazilah. Ni ukafiri mkubwa. Kupinga sifa za Allaah ni ukafiri mkubwa. Kwa sababu ni kumkadhibisha Allaah na ni kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ambaye anasema kuwa Allaah hana rehema, hasifiwi utukufu, hasifiwi kuwa na msamaha ni ukafiri mkubwa.

Swali: Vipi ikiwa anazipindisha maana?

Jibu: Yote ni ukafiri mkubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21526/حكم-التاويل-في-صفات-الله-تعالى
  • Imechapishwa: 22/08/2022