Hukumu ya kuzikata nywele za wasichana kwa sababu ya usumbufu wa kusukwa

Swali: Mwanamke huyu anasema kuwa alizikata nywele za mtoto wake wa kike ambaye ana miaka tano ukataji unaofanana na nywele za mtoto wa kiume. Sababu ya kufanya hivo ni kwa kuwa msichana huyu anakataa kuzifunga nywele zake, jambo ambalo linafanya nywele zake kutoonekana vizuri. Je, nina dhambi kwa kufanya hivi? Je, kujifananisha na jinsia nyingine ambako kumaharamishwa kunamuhusu tu mwanamke ambaye kishabaleghe au hata kwa watoto pia?

Jibu: Mwanamke huyu ni mwenye kupata dhambi kwa kufanya hivi. Anapata dhambi kupunguza nywele za msichana wake mpaka zikawa ni zenye kufanna na nywele za mtoto wa kiume. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke mwenye kujifananisha na mwanaume. Ni wajibu kwa mtoto kujiepusha na yale anayojiepusha nayo mkubwa. Mtoto hapati dhambi kwa sababu kalamu yake haijaanza kufanya kazi. Lakini ni yule mlezi wake ndiye mwenye kupata dhambi pale atapofanya yale yaliyo haramu kwa mkubwa. Ikiwa msichana huyu asipokatwa nywele zake zitaonekana vibaya  namna hii afadhali iwe hivyo. Mtu hatakiwi kufanya kitu cha haramu kwa ajili eti ya kutengeneza nywele. Ni wajibu kwa mwanamke huyu kutubu kwa Allaah na asirudi kufanya kitu kama hicho. Vinginevyo anapata dhambi. Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema:

“Waamrisheni watoto wenu swalah wanapofikisha miaka saba?”

pamoja na kuwa katika umri huu swalah sio lazima kwao. Lakini msimamizi anatakiwa kuwalea watoto kwa mujibu wa yale yanayomridhisha Allaah na Mtume wake. Hapa inahusu katika kufanya yale yaliyoamrishwa na kujiepusha na yale yaliyoamrishwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/705
  • Imechapishwa: 28/10/2017