Swali: Ni ipi hukumu ya kuwatukana maiti? Je, kitendo hicho kinamuudhi au kina taathira kwake?

Jibu: Kumekuja makatazo ya kuwatukana maiti kwa sababu wameshayaendea yale waliyoyatenda. Haijuzu kuwatukana maiti isipokuwa ikiwa katika kuwataja kuna manufaa ya Kishari´ah. Kwa mfano maiti huyu ni miongoni mwa wanachuoni wa upotevu au ana athari mbaya. Hivyo italazimika kuwazindua waislamu juu ya athari yake na upotevu wake ili watahadhari juu ya hilo. Ama kuwasema vibaya tu ni jambo la usengenyi. Jengine kuwatukana tu ni kitu kisichokuwa na manufaa nyuma yake na hivyo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/377)
  • Imechapishwa: 04/01/2020