Hukumu ya kuwapiga vita ISIS


Swali: Wamepewa mtihani na ISIS Iraaq na wanauliza ni ipi hukumu ya kuwapiga vita?

Jibu: Inavyoonekana – na Allaah ndiye Anajua zaidi – ni kwamba kundi hili ni shambulizi, dhalimu na lilivoka mipaka; wanamwaga damu, wanavunja heshima za watu na wanaporaji mali. Hili ni kundi limepitiliza, lilo la madhara na lenye kuudhi huko walipopata nguvu. Kuna watu wajinga wanafikiria kuwa ni sahihi wanavovunja heshima za watu na kuwafanya wanawake kuwa watumwa wanaouwauza kana kwamba ni wajakazi na kutangamana nao katika mambo yote kama makafiri. Hili ni kundi pasina shaka lenye dhambi. Haliko katika usawa. Wakiwapiga vita Waislamu, Waislamu nao wanatakiwa kuwapiga vita ili waweze kusalimika na shari zao. Hii ni shari na balaa. [Sauti haiko wazi]. Uuaji wao una ukeketaji, unyama na sura mbaya. Wanafanya matendo yanayowapa watu kinyaa. Kutokana na yale yanayoonekana katika vyombo vya khabari matendo yao ni ya khatari sana na machafu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/PNnRT0dVtZE
  • Imechapishwa: 15/11/2014