Hukumu ya kuuza bidhaa kwa sherehe za makafiri

Ni jambo la kuchukiza kabisa (Makruuh) kufanya biashara na kusafiri katika miji ya maadui na makafiri. Ibn Hamdaan anasema:

“Hali kadhalika hili linahusiana na [miji] ambayo Khawaarij, waasi, Rawaafidhw na za wapotofu wazushi.”

Shaykh Taqiyy-ud-Diyn [bin Taymiyah] kasema:

“Ahmad kasimulia mapokezi mawili juu ya kufanya biashara katika miji ya makafiri ambapo mtu hana mkataba nao (Daar-ul-Harb). Kufanya biashara pamoja nao kwa vitu vya chakula, mavazi na mfano wa hayo wakati wa sherehe zao inamaanisha kuwa mtu anasaidiana nao kabisa kwa sherehe zao na dini.”

Katika tukio lingine, kataja chaguzi mbili tofauti na kwamba kauli yenye nguvu ni kuwa haijuzu. ‘Abdul-Maalik kasema katika “al-Waadhwihah” kwamba hii pia ndio kauli ya Maalik. Hali kadhalika ni tabia mbaya ya kusaidia dini yao. Ama kuhusiana na mauzo ya silaha katika Daar-ul-Harb, haijuzu jambo ambalo limetajwa katika vitabu vya Fiqh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muflih al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Aadaab ash-Shar’iyyah (3/418-419)
  • Imechapishwa: 06/10/2020