Hukumu ya kuua nzi na mbu kwa vifaa vya umeme vya kisasa

Swali: Ni ipi hukumu ya kuua nzi kwa vifaa vya umeme pamoja na kuzingatia kwamba vifaa vya umeme vimeenea misikitini?

Jibu: Bora ni mtu asiue kwa umeme. Kwa sababu umeme ni aina fulani ya moto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haadhibu kwa moto isipokuwa Muumba wa moto.”

Nzi ziuawe kwa kitu kingine kama madawa na mfano wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10)
  • Imechapishwa: 13/04/2019