Hukumu ya kutukufu kwenye kaburi la maiti

Swali: Kutufu kwa kulizunguka kaburi ikiwa mtu haitakidi kuwa linanufaisha na kudhuru lakini hata hivyo anakusudia kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanah) ahukumiwe ukafiri?

Jibu: Ndio. Ni kufuru. Ni kama mfano wa anayeswali kwa ajili yao. Ni kufuru kubwa. Ni kama mfano wa anayeswali kwa ajili yao, akawaomba, akawataka uokozi, akaitakidi kuwa ni waombezi kwa njia ya kwamba akawa anawaomba, sio kwa sababu wanaumba, wanaruzuku au wanaendesha mambo. Bali akawa anawaomba tu ili wamuombee. Hii ni kufuru kubwa.

Ama endapo atatufu kwa kufikiria kuwa ni jambo lililowekwa katika Shari´ah na akasema kuwa malengo yake ni Allaah na yeye hawalengi wao na kwamba anatukufu kwa kumkusudia Allaah kwa kufikiria kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah, kama mfano wa kutukufu Ka´bah, hii ni Bid´ah na njia inayopelekea katika shirki. Hili ni mara chache kutokea. Wengi wanaotukufu wanakusudia kujikurubisha kwa yule aliyomo ndani ya kaburi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 18/11/2016