Hukumu ya kuswali Maghrib kabla ´Aswr iliyompita mtu


Swali: Kuna mtu amepitwa na swalah ya ´Aswr na alipokuja msikitini akakuta watu wameanza kuswali Maghrib. Je, aanze kuswali ile swalah iliyompita kabla ya Maghrib au hapana?

Jibu: Aswali Maghrib pamoja na imamu. Kisha aswali ´Aswr kwa maafikiano ya maimamu. Lakini je, arudi kuswali swalah ya Maghrib? Hakuna maoni mawili:

Ya kwanza: Airudi. Haya ni maoni ya Ibn ´Umar, Maalik, Abu Haniyfah na Ahmad katika maoni yaliyotangaa kwake.

Ya pili: Hatoirudi Maghrib. Haya ni maoni ya Ibn ´Abbaas, ash-Shaafi´iy na Hanaabilah katika maoni yao mengine.

Haya maoni ya pili ndio sahihi zaidi. Kwa sababu Allaah hakumuwajibishia mja kuswali swalah moja mara mbili midhali amemcha Allaah kiasi na uwezo wake – na Allaah ndiye mwenye kujua zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (22/106)
  • Imechapishwa: 03/03/2019