Hukumu ya kushirikisha katika nia

Swali: Ni ipi hukumu ya kushirikisha katika nia?

Jibu: Vipi atashirikisha katika nia? Ikiwa atakusudia kwa kitendo chake asiyekuwa Allaah kuanzia katika msingi wake basi jambo hili ni khatari. Ama ikiwa msingi wa kitendo kimefanywa kwa ajili ya Allaah kisha baadaye kikaingiliwa na kujionyesha haidhuru. Ama ikiwa hali hiyo itaendelea basi yuko khatarini juu ya kubatilika kwa kitendo chake hicho.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2018