Hukumu ya kusawazisha safu

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kuzisawazisha swalah ni katika utimilifu wa swalah.”

Je, maneno haya si yanaigeuza amri hii kutoka katika ulazima kwenda katika mapendekezo?

Jibu: Hapana, hayaigeuzi. Utimilifu wa swalah bi maana kitu kinachoifanya kukamilika. Kusawazisha safu ni sehemu katika kuikamilisha swalah. Swalah isipokamilika haisihi. Rak´ah ikipungua tunasema kuwa haikusihi. Kwa hivyo haifahamishi kupendekeza. Kukamilika kwa swalah bi maana kitu kinachoikamilisha na wala haisihi isipokuwa kwa kukifanya. Wako baadhi ya wanachuoni wameitumia kwamba kutosawazisha safu kunaharibu swalah. Maoni ya sawa ni kwamba kusawazisha safu ni wajibu. Lakini hata hivyo hakuiharibu swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/69/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%B3%D9%88%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%81%D9%88%D9%81
  • Imechapishwa: 27/12/2019