Hukumu ya kupwekesha funga siku ya ´Aashuuraa´

Swali: Mimi nina mtoto ambaye ana miaka kumi alifunga siku ya ´Aashuuraa´ na wala hakufunga kabla yake wala baada yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Ibn ´Uthaymiyn: Mashaa Allaah! Ana miaka kumi tu?

Muulizaji: Ndio, ana miaka kumi tu.

Ibn ´Uthaymiyn: Hakuna neno kwake. Kwa sababu kufunga siku moja kabla yake au baada yake ni kwa njia ya ubora tu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1738
  • Imechapishwa: 03/09/2020