Hukumu ya kupeana hongera katika mwaka mpya wa Kiislamu

Swali: Umezungumzia kuhusu mwaka mpya. Ni ipi hukumu ya kupeana hongera juu ya mwaka wa al-Hijriyyah? Tunatakiwa kuchukua msimamo gani juu ya wale wanaopeana hongera?

Jibu: Akikupa hongera mtu basi nawe mrudishie. Usianze kumpa yeyote juu ya hilo. Huu ndio usawa katika masuala haya. Kwa mfano mtu akikwambia:

“Nakupea hongera ya mwaka mpya.”

Nawe mwambie:

“Allaah atupe kheri na Allaah ajaalie iwe ni mwaka wa kheri na baraka.”

Lakini wewe usianze kuwapa watu. Kwa sababu sijui kama imekuja kutoka kwa Salaf kwamba walikuwa wakipeana hongera kwa mwaka mpya. Bali najua kuwa Salaf hawakuuchukua mwezi wa Muharram au mwanzo wa mwaka mpya isipokuwa katika uongozi wa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) al-Liqaa’ ash-Shahriy (43) http://binothaimeen.net/content/985
  • Imechapishwa: 13/01/2019