Swali: Ni ipi hukumu ya an-Nushrah? Kwani tumewasikia wenye kusema kuhusu hilo kwamba dharurah inapelekea kuruhusu kilichoharamishwa. Je, kanuni hii inatumika katika mambo yote yenye dharurah? Allaah akujaze kheri.

Jibu: an-Nushrah ni kuondosha uchawi kutoka kwa yule aliyefanyiwa uchawi. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amegawanya an-Nushrah mafungu mawili:

1- an-Nushrah kwa kuomba du´aa mbalimbali kama za kuomba ulinzi na kisomo. Hii inafaa. Haina utatizi wowote.

2- an-Nushrah kwa kutumia uchawi kwa njia ya kwamba mtu akaenda kwa wachawi ambao wakamwelekeza ni wapi unapatikana uchawi aliyofanyiwa. Amesema kuhusu aina hii:

“Ni katika matendo ya shaytwaan na kwamba haijuzu.”

Kuhusu maneno ya wenye kusema kwamba dharurah inapelekea kuruhusu kilichoharamishwa, haihusiani na kuruhusu kitu kilichofungamana na ´Aqiydah. Mnasemaje mgonjwa akiambiwa kwamba hawezi kupona isipokuwa mpaka azini. Inafaa akazini? Hawezi kuzini. Kwa sababu miongoni mwa sharti za kuruhusu kitu kilichoharamishwa wakati wa dharurah ni dharurah iondoshe kitu hicho. Kwa hali yoyote masuala haya Ibn-ul-Qayyim ameyagawanya katika mafungu mbalimbali. Yule anayetaka kusoma zaidi kuhusu hayo basi arudi katika “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Ametaja mlango wa pekee kuhusu haya na akasema:

“Mlango kuhusu an-Nushrah”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1342
  • Imechapishwa: 18/11/2019