Hukumu Ya Kuogopa Maradhi Ya Khatari

Swali: Ni ipi hukumu ya kuogopa maradhi ya khatari?

Jibu: Hii ni khofu ya kimaumbile. Jitunze na ufanye sababu za kujikinga nayo. Hii ni khofu ya kimaumbile na sio khofu ya ´ibaadah. Wewe unaabudu magonjwa? Hapana. Una khofu ya kimaumbile ili yasije kukusibu. Jitunze na ufanye sababu za kujikinga nayo. Fuata ushauri wa madaktari na ujikinge nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017