Swali: Baadhi ya watu wazuri wameoa baadhi ya wanawake wachafu au kinyume chake…

Jibu: Hili haliwezekani. Hili haliwezekani – in shaa Allaah. Wanawake wachafu bi maana wazinifu. Muislamu hawezi kumuoa mwanamke mzinifu.

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ

“Mzinifu mwanamme hafungamani (hafungi Nikaah) isipokuwa na mzinifu mwanamke au mshirikina mwanamke; na mzinifu mwanamke hafungamani naye (haolewi na yeyote) isipokuwa na mzinifu mwanamme au mshirikina mwanamme.” (02:286)

Wala sio sahihi kumuoa. Isipokuwa akitubu na Zinaa na akatoka katika eda, anaweza kuolewa. Lakini maadamu bado hajatubia na Zinaa, sio sahihi na wala haijuzu kumuoa. Ni (ndoa) batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13832
  • Imechapishwa: 16/11/2014