Hukumu ya kumlazimisha msichana kuolewa

Swali: Kuna mtu ambaye amemuozesha ndugu yake msichana wake wa kulea na msichana mwingine wa kulea anamlazimisha aolewe na mtoto wake. Lengo la yeye kufanya hivo ni kwamba wasichana hawa wana pesa nyingi. Amewalazimisha kuolewa na ndugu na mtoto wake pamoja na kuzingatia kwamba wanaishi kwenye nyumba ndogo tokea walipokuwa wadogo. Je, ni haki au batili?

Jibu: Si haki kwa mlezi yeyote yule kumlazimisha anayemlea juu ya kuolewa. Haijalishi kitu hata akiwa baba mwenyewe. Si haki kwake kumlazimisha msichana wake yule ambaye hataki kuolewa naye. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiozeshwe msichana bikira mpaka atakwe idhini.”

Hakupambanua (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kati ya baba na mwengineo wala baina ya msichana bikira na mwengineo. Katika “as-Swahiyh” ya Muslim imekuja:

“Msichana bikira anaamuriwa na baba yake.”

Amemtaja msichana bikira na baba. Hiyo ni dalili inayofahamisha kwamba ni lazima kwa mwanaume kumtaka idhini yule mlezi anayetaka kumuozesha. Ni mamoja akiwa ni baba, kaka, baba mkubwa au mdogo au mtoto wake. Ni lazima amtake idhini juu ya hilo. Kutokana na haya mtu huyu ambaye alikuwa ni mlezi wa wasichana hawa haijuzu kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6707
  • Imechapishwa: 12/11/2020