Hukumu ya kulala na janaba pasi na kutawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye amemwingilia mkewe akalala pasi na kutawadha wala kuoga? Anapata dhambi kwa kufanya hivo?

Jibu: Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba imechukizwa sana. Wakati ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, mmoja wetu aoge ilihali ana janaba?” Akajibu: “Ndio, pindipo atatawadha.”

Kwa hivyo anatakiwa kutawadha[1]. Kile kitendo chake cha yeye kulala pasi na angalau kutawadha imechukizwa sana.

Tazama https://firqatunnajia.com/12-wenye-janaba-wanatakiwa-kutawadha-kabla-ya-kulala/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 14/04/2018