Swali: Familia yangu inasherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kupika chakula maalum katika siku hiyo. Je, inajuzu kwangu kula chakula hicho?

Jibu: Hapana, bali ni wajibu kuwakumbusha kwa kuwa kusherehekea maulidi ya Mtume ni Bid´ah iliyozushwa. Hakufanya hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aliishi miaka ishirini na tatu huku ni Nabii na Mtume na wala hakusherehekea kuzaliwa kwake. Makhaliyfah waongofu na Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na karne bora na wanachuoni, wote hawakufanya maulidi. Bali ni Bid´ah na upotofu. Waliyozua Bid´ah hizi ni wapotofu. Kutolewe tahadhari kwa wale wanaopeana nguvu waliyoathirika kwa kula chakula cha maulidini na kusherehekea sikukuu zao, bali awabainishie haki kuhusiana na hilo na kuwapa nasaha kuwa Bid´ah ni khatari kwa watu wake, na miogoni mwazo ni kusherehekea maulidi. Na hili ni katika uongo kwa kuwa Allaah kishaeleza kuwa mwenye kufa harejei duniani, si Mtume wala aliye chini yake mpaka Qiyaamah kitapofika. Wao wanadai kuwa Mtume anahudhuria sherehe zao na anawabarikia, bali anawasamehe hata madhambi zao. Na hili ni katika maovu makubwa, na wamelifanya al-Ikhwaan al-Muslimuun kama Hasan al-Bannaa na watu mfano wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Zayd al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2TYsJPMtUgQ
  • Imechapishwa: 21/08/2021