Hukumu ya kukusudia kuchelewesha Zakaat-ul-Fitwr

Swali: Kuna mtu amechelewesha Zakaat-ul-Fitwr mpaka ukatoka wakati wake kwa kukusudia. Je, ni lazima kuitoa hali ya kuwa ni mwenye kuilipa au inakatika kwake?

Jibu: Hapana, haikatiki kwake. Anatakiwa kuitoa pamoja na kupata madhambi. Aitoe hali ya kuwa ni mwenye kuilipa na anapata madhambi kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-1-24.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014