Hukumu ya kukaa sehemu ya mwingine katika vikao vya elimu

Swali: Kuna baadhi ya watu wanakuja wamechelewa na wanaketi sehemu za wenzao, wanatenganisha vitabu vyao au wanaweka vitao vyao sehemu finyu. Tunaomba uwape nasaha?

Jibu: Mtu anatakiwa kuketi pale kikao kilipoishilia. Mtu aliyetangulia katika sehemu ana haki zaidi ya sehemu hiyo. Hakuna haja ya kujibana. Wanafunzi wanatakiwa kuoneana huruma, upole na kupendeleana. Lakini yule mwenye kutangulia ana haki zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2018