Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewazungumzisha waumini kujiepusha kuyafanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Tunaona baadhi ya misikiti imejengwa juu ya makaburi ya Mitume na wanachuoni waliotangulia katika Uislamu. Je, inafaa kufanya hivi?

Jibu: Kinachopata kufahamika katika siyaaq ya swali ni kwamba makatazo ya kufanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia ni jambo limekuja katika Uislamu. Kwani muulizaji amesema:

“Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewazungumzisha waumini kujiepusha.”

Udhahiri wa swali ni kwamba hayo yamo ndani ya Qur-aan, mambo si kama alivyodhania ikiwa ndivo alivodhania. Haya hayamo ndani ya Qur-aan. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wale wenye kuyafanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hayo yamekuja katika Sunnah.

Hapana shaka kwamba kuyafanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia ni dhambi kubwa. Lakini kaburi likipatikana ndani ya msikiti, ikiwa msikiti umejengwa juu ya kaburi basi ni wajibu kuubomoa na kuuondosha. Ikiwa kaburi liliwekwa msikitini baada ya kujengwa kwa msikiti, basi ni wajibu kuliondosha nje ya msikiti. Kwa hiyo hukumu inategemea na ni kipi kilichoanza katika hivyo viwili. Ikiwa kitu cha kwanza kilichoanza ni msikiti, basi kaburi litaondoshwa. Ikiwa kitu cha kwanza ilikuwa kaburi, basi msikiti utavunjwa. Haijuzu kuijenga misikiti juu ya makaburi. Wala haijuzu kuwazika wafu ndani ya msikiti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (02) http://binothaimeen.net/content/6635
  • Imechapishwa: 09/03/2019