Hukumu ya kufanyiwa chanjo kabla ya kupatwa na ugonjwa

Swali: Ni ipi hukumu ya kujitibisha, kama kufanyiwa chanjo, kabla ya kutokea magonjwa yenyewe?

Jibu: Hakuna neno kufanya matibabu pindi mtu anapochelea kutokea kwa magonjwa kwa kupatikana magonjwa ya mlipuko au sababu nyenginezo ambazo mtu anachelea kusitokee magonjwa kwa sababu yake. Hakuna neno kutumia dawa kwa sababu ya kuzuia janga analochelea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth ambayo ni Swahiyh:

”Yule ambaye atapambaukiwa asubuhi kwa kula tende saba katika tende za Madiynah basi hatodhuriwa na uchawi wala sumu.”

Haya ni kwa minajili ya kuzuia janga kabla ya kutokea kwake. Vivyo hivyo akiogopa maradhi au tauni dhidi ya magonjwa ya mlipuko yaliyotokea nchini au mahali kokote, basi hakuna neno kufanya hivo kwa njia ya kujikinga. Ni kama ambavo yanatibiwa maradhi yaliyozuka ambayo mtu anachelea kwa dawa.

Hata hivyo haijuzu kutundika hirizi dhidi ya maradhi, majini au kijicho. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Ameliingiza hilo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya shirki ndogo. Kwa hivyo ni lazima kutahadhari jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/26)
  • Imechapishwa: 09/02/2021