Swali: Nimesikia kutoka kwa baadhi ya watu kwamba haijuzu kuapa kwa sifa za Allaah na khaswakhaswa sifa ya uhai wa Allaah. Nikawaambia kwamba kuapa kwa uhai wa Allaah inafaa kujengea yale niliyosoma. Je, maneno yangu ni sahihi?

Jibu: Ndio, kuapa kwa sifa na majina ya Allaah inajuzu. Kama mfano wa ilivyokuja katika Hadiyth:

أعوذ بعزة الله وقدرته من شر ما أجد وأحاذر

“Najilinda kwa nguvu na uwezo wa Allaah kutokamana na shari ya kile ninachohisi na kuogopa.”

أعوذ برضاك من سخطك

“Najilinda kwa radhi Zako kutokamana na ghadhabu Zako.”

أعوذ بكلمات التامات

“Najilinda kwa maneno yaliyotimia.”

Kwa hivyo kuapa kwa sifa na majina ya Allaah yote hayo yanafaa. Inafaa kwa mtu akaapa kwa jina la Allaah, sifa Zake na majina Yake. Kama mfano wa nguvu za Allaah, uwezo wa Allaah na uhai wa Allaah. Yote hayo yanajuzu. Ni kama anavosema “Ninaapa kwa Allaah”, “Ninaapa kwa Mwingi wa huruma”, “Ninaapa kwa Mwingi wa kurehemu”, “Ninaapa kwa Mshindi na kwa Mwingi wa hekima”. Yote haya yanajuzu. Vivyo hivyo akisema “Ninaapa kwa nguvu za Allaah”, “Ninaapa kwa ujuzi wa Allaah” na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=qqNj1OB0Vdw
  • Imechapishwa: 06/10/2018