Hukumu ya kuandika Khutbah na imamu akhutubu

Swali: Nimewaona baadhi ya watu wanaandika kwa ufupi Khutbah ya ijumaa wakati uko unakhutubu. Je, kitendo hichi ni sahihi?

Jibu: Kitendo hichi si sahihi. Kwa sababu akiandika kwa ufupi sentesi ya maneno atapitwa na sentesi nyingine au akaandika kwa njia ya makosa. Kwa hivyo si ruhusa kwa mtu kuandika kwa ufupi Khutbah ya ijumaa. Lakini hapa kuna jambo muhimu zaidi kuliko hili; kuna vitu vyenye kurekodi. Aweke kitu chenye kurekodi kidogo sana na arekodi. Atakapoenda nyumbani aandike kwa ufupi anayotaka. Kwa hivyo usiandike si vidogo wala vingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1551
  • Imechapishwa: 22/02/2020