Hukumu ya kuacha kufanya matendo kwa kuchelea kujionyesha

Swali: Mwenye kuacha kufanya matendo kwa sababu ya watu anakuwa mwenye kujionyesha? Kwa mfano mtu ana mazowea ya kusimama usiku na kuswali. Mtu huyo akatoka pamoja na wengine ambao hakuna yeyote mwenye kusimama usiku. Matokeo yake akaacha kusimama usiku kwa kuchelea asijionyeshe.

Jibu: Wanachuoni wamesema kwamba mtu kufanya matendo kwa sababu ya watu ni shirki na kuacha kufanya matendo kwa sababu ya watu ni shirki pia. Aliyesalimika ni yule aliyesalimishwa na Allaah katika hao wawili.

Ni lazima kwa mtu kupambana na nafsi yake na asiache matendo. Akiacha kufanya matendo kwa sababu ya watu inakuwa ni kujionyesha na akifanya matendo kwa ajili ya watu ni kujionyesha. Ni lazima kwa mtu kupambana na nafsi yake na amtake msaada Allaah na asiache matendo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 22/06/2019