Hukumu ya josho la siku ya ijumaa


Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu zaidi juu ya josho la siku ya ijumaa? Imependekezwa au ni lazima?

Jibu: Maoni yenye nguvu zaidi ni kwamba limekokotezwa. Lakini hata hivyo ni jambo limekokotezwa sana, ni Sunnah isiyotakiwa kuachwa. Lakini sio lazima. Hakuna waliosema kuwa ni lazima isipokuwa wanazuoni wachache wakiwemo Dhwaahiriyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 05/02/2022