Hukumu ya jina la ´Abdul-Muttwalib


Swali: Je, inajuzu kuitwa kwa jina la ´Abdul-Muttwalib?

Jibu: Ibn Hazm (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wameafikiana juu ya uharamu wa kila jina ambalo lina uabudiwa kwa asiyekuwa Allaah isipokuwa ´Abdul-Muttwalib.”

Anaonelea kuwa inajuzu.

Kadhalika nimemsikia Shaykh Ibn Baaz mara mbili au mara tatu kwamba inajuzu. Lakini katika nafsi yangu mimi kuna kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (71) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13910
  • Imechapishwa: 16/11/2014