Hukumu ya damu pindi inapoharibika mimba ya mwanamke

Swali: Ni ipi hukumu ya damu ikiharibika mimba ya mwanamke? Je, huzingatiwa ni damu ya uzazi au damu ya hedhi?

Jibu: Ikiwa kuharibika kwa mimba ni baada ya kuumbwa mtoto na ikabaini kwamba ni mtu, kwa mfano kukabaini kichwa au mkono ijapo itakuwa ni kiungo kilichojificha, basi hiyo ni damu ya uzazi. Katika hali hiyo ni lazima kwa mwanamke kuacha kuswali na kufunga mpaka asafike au akamilishe siku arobaini. Kwa sababu hicho ndio kikomo cha muda ya uzazi. Akisafika kabla ya hapo basi ni lazima kwake kuoga, kuswali, kufunga na ni ni halali kwa mumewe. Damu ikiendelea basi ataacha kuswali na kufunga na hatokuwa halali kwa mumewe mpaka akamilishe siku arobaini. Akizikamilisha basi ataoga, atafunga, ataswali na atahalalika kwa mumewe ijapo atakuwa bado yuko na damu. Kwa sababu damu hiyo katika kipindi hicho itazingatiwa ni damu ya kwaida. Kile kinachozidi juu ya siku arobaini huzingatiwa ni damu ya kawaida. Hivyo atatakiwa kutawadha kwa ajili ya kila swalah pamoja na kujihifadhi kama mfano wa mwenye damu ya ugonjwa na ambaye hawezi kudhibiti mkojo wake.

Lakini akiwa bado hajaumbwa na hakujaonekana kwake kinachojulisha umbile la mtu, kwa mfano ni kipande cha nyama ambacho hakina umbile la mtu au akatokwa na damu peke yake, basi hiyo huzingatiwa ni damu ya kawaida. Hivyo atatakiwa kuswali, kufunga na kutawadha juu ya kila swalah na ajihifadhi vizuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/228)
  • Imechapishwa: 09/09/2021