Swali: Mwanamke mjamzito anatokwa na damu. Ni ipi hukumu ya swalah zake na swawm yake? Je, aache kuswali na kufunga?

Jibu: Mwenye mimba akitokwa na damu, basi damu hiyo ni fasidi na sio hedhi. Hivyo aswali na swalah yake ni sahihi. Afunge na funga yake ni sahihi. Ni halali kwa mume wake  yale ambayo ni halali kwake wakati anapokuwa hana damu hii. Kwa sababu damu hii wanachuoni wanaiita kuwa ni damu ´fasidi`.

Lakini asitawadhe kwa ajili ya kuswali isipokuwa baada ya kuingia wakati wa swalah hiyo. Isipokuwa swalah za sunnah wakati atapotaka kuswali basi atawadhe. Haijalishi kitu ni wakati gani mbali na zile nyakati zilizokatazwa. Kuhusu swalah za faradhi asitawadhe isipokuwa baada ya kuingia wakati. Hapa ni pale ambapo damu itakuwa ni yenye kuendelea. Ama ikiwa ni yenye kukatika na akatawadha na asitokwe na kitu mpaka ukaingia wakati wa swalah, basi aswali swalah yake na hakuna neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1220
  • Imechapishwa: 01/09/2019