Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kudai kuwa kuna ambao wamekingwa na kukosea mbali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hukumu yake ni kuwa amekosea. Isipokuwa ikiwa kama yuko na elimu au amebainishiwa haki lakini pamoja na hivyo akaendelea kung´ang´ania anahukumiwa ukafiri. Kwa kuwa amemsawazisha mwengine na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo anaweza kupewa udhuru kwa ujinga, kufuata kichwa mchunga na mfano wa nyudhuru zingine kama hizo. Ni lazima kubainisha na kutokuwa na haraka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 30/01/2017