Hukumu ya an-Najaashiy si dalili

Swali: Baadhi ya watu wanategemea kiasi cha an-Najaashiy na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsifia ilihali hakuhukumu kwa Shari´ah. Wanasema kuwa huo ni udhuru wa kuhukumu kwa kanuni hii leo. Je, utumiaji wa dalili huu ni sahihi?

Jibu: an-Najaashiy alikuwa katika nchi ya kinaswara na hakuingia katika Uislamu. Asingeweza kutendea kazi Uislamu kwa kuzingatia kwamba hakuwa muislamu. Ni mwenye kupewa udhuru kwa njia hiyo.

Kuhusu wale ambao wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na wanajinasibisha na Uislamu, basi ni lazima wahukumu kwa Shari´ah. Kwa sababu wanaiamini.  Wanashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah na wanaimini Qur-aan na Sunnah. Kwa hivyo ni lazima waitendee kazi Shari´ah.

Kuhusu kuitendea kazi juu ya makafiri… Ni vipi utaitendea kazi kwa makafiri ilihali hawaiamini?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10306
  • Imechapishwa: 14/03/2021