Hukumu ya aliyechelewa ambaye hakumfuata imamu katika sujudu ya kusahau

Swali: Niliswali pamoja na imamu na nilikuwa nimechelewa. Imamu alipotoa Tasliym nikasimama kwa ajili ya kulipa. Tahamaki imamu akasujudu sujudu ya kusahau baada ya Tasliym lakini hata hivyo sikumfuata katika sujudu yake ya kusahau na wala sikusujudu baada ya kumaliza kulipa kwangu. Je, kuna jambo linalonilazimu? Je, nirudi swalah yangu?

Jibu: Ni lazima kwako kusujudu sijda mbili pindi utakapomaliza kulipa yale yanayokuwajibikia hata kama muda utakuwa umeshapita mrefu. Mtu akiacha kufanya hivo ima kwa ujinga au kwa kusahau basi wanachuoni wanaona kuwa sijda mbili hizo zinaanguka ikiwa muda umeshapita mrefu au wudhuu´ ukamchenguka. Lakini lililo bora zaidi ni kwamba pindi atapokumbuka basi asujudu hata kama muda utakuwa umeshapita mrefu. Kinachokusudiwa ni kwamba hakuna kinachokulazimu. Ikiwa utasujudu wakati wowote ni sawa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 17/03/2019