Hukumu ya wanawake kupaka sehemu ya nywle za kichwani rangi

Swali: Inajuzu kupaka rangi sehemu ya nywele kama kwa mfano mtu akapaka ncha au zile nywele zilizoko juu peke yake?

Jibu: Ikiwa kupaka rangi nywele ni kwa rangi nyeusi basi hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelikataza hilo pale alipoamrisha kuzibadilisha mvi na mtu ajiepushe na rangi nyeusi:

“Zibadilisheni mvi hizi na jiepusheni na [rangi] nyeusi.”

Isitoshe kumepokelewa makemeo juu ya yule mwenye kufanya hivi. Ni dalili inayothibitisha uharamu wa kuzibadilisha nywele kwa rangi nyeusi.

Ama kuzibadilisha kwa rangi nyingine kimsingi ni kwamba inafaa. Isipokuwa ikiwa ni kwa kujifananisha na wanawake wa kikafiri au watenda madhambi. Itakuwa ni haramu kwa upande huo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/120)
  • Imechapishwa: 28/06/2017