Hukumu ya kujitoa manii


Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya punyeto kwa bikira na ambaye kishaoa? Ni ipi njia bora kwa mtu kuachana nalo?

Jibu: Haijuzu kufanya punyeto, sawa kwa ambaye kishaoa na kwa ambaye hajaoa. Ni haramu. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ

“Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi.” (23:05-06)