Huku sio kwenda kinyume kuwafanyia uadilifu watoto

Swali: Kuhusu mada inayozungumzia kuwafanyia uadilifu watoto[1]. Baba akiwapa zawadi watoto waliofaulu na akawanyima waliofeli ni jambo linaloenda kinyume na uadilifu?

Jibu: Kitendo hichi hakiendi kinyume na uadilifu. Kuwapa kwake zawadi ni kwa lengo la kuwashaji´isha juu ya masomo na kuweka misingi. Wakifaulu wengine atawapa vilevile. Lakini endapo mmoja atafaulu katika darasa la kwanza na mwingine katika darasa la pili zawadi zitakuwa sawa? Hapana. Tukienda kwa uadilifu si sawa. Kwa sababu aliye katika darsa la kwanza yuko nyuma ukilinganisha na yule aliye katika darasa la pili.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/mavazi-ya-mwanamke-mbele-ya-wanawake-wenzie-na-maharimu-wake/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/816
  • Imechapishwa: 23/02/2018