Swali: Mwenye kuacha kufanya matendo mengi mema halafu anasema kuwa anamjengea dhana njema Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba Allaah ni Mwingi wa kusamaha na Mwingi wa huruma. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Huku ni kughurika. Si sahihi. Anatakiwa kutenda matendo mema na amdhanie Allaah vyema ya kwamba Allaah atayakubali na atamlipa kwayo. Ajenge dhana nzuri pamoja na kutenda na sio kujenga dhana nzuri kwa kutenda maovu. Huku ni kughurika ambapo mtu anajenga dhana nzuri na anaacha kufanya matendo kwa kudhani kuwa Allaah atamsamehe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018