Huku ni kufungua njia ya kuhuisha Bid´ah ya Maulidi

Swali: Siku hizi kumekithiri maongezi katika magazeti na TV na Khutbah za Ijumaa kwenye misikiti kuhusu historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na haki zake na tabia yake kwa sababu mazao yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yamekaribia. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi na ni ipi nasaha yako kwa Ummah juu ya hilo?

Jibu: Ndio, kuzungumzia historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tabia yake, kukumbusha juu ya kumpenda na kumfuata ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Lakini hata hivyo haitakiwi kulikhusisha na wakati fulani. Hili linafanywa wakati wote katika mwaka.

Kuhusiana na yule mwenye kukhusisha wakati huu na hazungumzii historia na sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa katika wakati huu, hii ni njia inayopelekea katika kuhuisha Bid´ah. Zindukeni juu ya hilo. Kukhusisha wakati huu ambapo ni karibu na kipindi cha Bid´ah, hii maana yake ni kushirikiana na watu wa Bid´ah katika kuhuisha Bid´ah.

Hakuna kitu kimechokufanya kukumbushia historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati huu isipokuwa ni kwa sababu kunataka kuhuishwa Bid´ah hii karibuni. Huyu anakuwa ni mwenye kushirikiana nao na kuwapa nguvu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2125
  • Imechapishwa: 05/07/2020