Swali: Mimi natumbukia kwenye dhambi kubwa kwa kuendelea. Lakini baada ya kufanya hivo ninatawadha, naswali Rak´ah mbili [Swalat-ut-Tawbah] na ninamuomba Allaah msamaha. Kisha narudi kufanya dhambi hiyo mara nyingine, natawadha na kuswali Rak´ah mbili na kuomba msamaha. Nifanye nini? Je, pale ninapotumbukia kwenye dhambi…

Jibu: Analotakiwa kufanya ni vile anavyofanya kwa yeye kutubu na asikate tamaa na rehema ya Allaah. Akariri tawbah. Kila pale ambapo anakariri dhambi akariri pia tawbah. Hii ni alama ya kheri kwa yeye kukariri tawbah na kumwogopa Allaah (´Azza wa Jall).

Swali: Je, kufanya hivi inahesabika kuwa ni kufanya mzaha?

Jibu: Hapana. Sio kufanya mzaha. Huku ni kumwogopa Allaah. Kule kukariri kwake tawbah ni dalili ya kuonesha kuwa anamwogopa Allaah na ndani ya moyo wake kuna hayaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_fitan%201-10-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015