Swali: Je, mtu ajifunze kupitia mikanda ya kielimu ambayo imefafanuliwa na wanachuoni katika miji ambayo hakuna wanachuoni kama fafanuzi zako na fafanuzi za Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)?

Jibu: Haifai kwa mtu kujifunza kupitia mikanda na vitabu. Lakini anachoweza mtu kufanya ni kufaidika kwavyo. Ama kujifunza kupitia mambo haya hapana. Lakini kule kusikiliza na kufaidika kwavyo ni sawa. Huku kunaitwa kufaidika na sio kusoma. Kusoma kunakuwa kwa kupitia kwa wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=uGzmaelIayM
  • Imechapishwa: 14/11/2017