Huko ndiko anatakiwa kukaa eda


Swali: Kuna mwanamke ambaye mume wake amekufa Baahah. Ana nyumba Baahah na nyumba nyingine Makkah. Anataka kwenda katika nyumba yake nyingine Makkah na kukaa eda huko. Inajuzu kwake kufanya hivo?

Jibu: Sio nyumba yake yeye. Ni nyumba ya mume wake. Anatakiwa kukaa eda katika nyumba ya mume wake na si nyumbani kwake. Anatakiwa kukaa eda katika nyumba ambayo mume wake kafa akiwa ndani yake mpaka pale eda yake itapokamilika. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baki nyumbani mpaka pale eda itakapomalizika.”

Bi maana eda ya kufiliwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 30/06/2018