Hoja ya Hizbiyyuun kwa kisa cha Yuusuf ili kuingia bungeni

Miongoni mwa aina ya mfumo huu magazeti ya ndani yalichapisha (nafikiri ilikuwa ni Shaykh ´Umar al-Ashqar ndiye aliandika) jinsi wanavotolea dalili kwa kisa cha Yuusuf (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba inajuzu kuwa waziri kwa kiongozi asiyehukumu kwa Shari´ah ya Allaah. Watu hawa wanajaribu kutafuta hoja kwa njia zote ziwezekanazo. Wanapopata kitu kwenye fikira zao basi hukitia kwenye mioyo yao, halafu wanataka kupata dalili zinazosapoti fikira zao. Lakini hakuna wanachoweza zaidi ya kwenda kinyume na dalili za wazi kabisa. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

 وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ

“Na chenye kuyadhibiti.” (05:48)

Allaah Anasema kuwa Qur-aan ni yenye kulinda vitabu vilivyokuwa kabla yake. Imepokelewa Hadiyth Swahiyh jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivoona sahifa kwenye mkono wa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anhu). Alipomuuliza juu yake akasema kuwa ni sahifa za Tawrat. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Ee mtoto wa Ibn Khattwaab! Je, mnatilia shaka kama walivotilia shaka mayahudu na manaswara? Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake; lau Muusa angelikuwa hai asingeliweza jengine isipokuwa kunifuata.”

Watu hawa hawakutosheka na Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayohukumu juu ya Shari´ah zingine zote. Pale waliposhindwa kupata katika Shari´ah kitu kinachosapoti upindaji wao ndio wakageuka kwenye Shari´ah ya Muusa na Yuusuf (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam).

Janga lingine ni kwamba wanajilinganisha na Mitume ambao wamekingwa na madhambi. Hili ni tatizo jingine. Kuna matatizo mawili. Wanategemea misingi ambayo haikuwekwa katika Shari´ah na wanajilinganisha na Mitume ambao wamekingwa na madhambi. Lau ingelikuwa ni janga moja tu. Kuna majanga mawili na huenda kukawa mingine iliyojificha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930) Tarehe: 1417-04-09/1996-08-24
  • Imechapishwa: 30/08/2020