Hoja ya Allaah, hoja ya Uislamu na alama ya Allaah

Swali: Ni ipi hukumu ya majina haya hoja ya Allaah (حجة الله), hoja ya Uislamu (حجة الإسلام) na alama ya Allaah (أية الله)?

Jibu: Majina haya hoja ya Allaah na hoja ya Uislamu ni majina yaliyozuliwa na yasiyotakikana. Kwa sababu hakuna hoja ya Allaah juu ya waja isipokuwa Mtume.

Kuhusu Aayah ya Allaah, ikiwa anakusudia ile maana iliyoenea basi naye anaingia katika kila kitu:

Katika kila kitu ipo alama

inayojulisha ya kwamba Yeye ni Mmoja

Ikiwa anakusudia kuwa yuko na miujiza, basi kitu hicho kinakuwa mikononi mwa Mitume. Mwanachuoni anaambiwa kuwa ni ´Aalim, Muftiy, Qaadhwiy, hakimu na Imaam kwa ambaye anastahiki maneno hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Manaahiy al-Lafdhwiyyah, uk. 36
  • Imechapishwa: 09/08/2022