Hoja imewasimamia watu kwa kufikiwa na Mitume

Swali: Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa Aayah ya ahadi:

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ

“Wakati Mola wako alipochukua katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao: “Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia [ili] msije kusema Siku ya Qiyaamah “hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya au mkasema “hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?” (07:172-173)

ya kwamba ni hoja dhidi ya watu hata kama hoja haikuwafikia hoja ya kiujumbe haikuwafikia. Je, haya ni sahihi?

Jibu: Si sahihi. Hoja inawasimamia watu kwa kufikiwa na Mitume. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

“Hatukuwa ni wenye kuadhibu mpaka Tupeleke Mtume.” (17:15)

Kuhusu Aayah ya ahadi Mitume ndio wanatakiwa kuwakumbusha juu ya ahadi hii. Lakini ahadi yenyewe haitoshi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67955&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 20/08/2017