Swali: Je, kuna aina ya Tawhiyd inayoitwa Tawhiyd-ul-Haakimiyyah au inaingia katika aina tatu za Tawhiyd?

Jibu: Hii imezushwa na Hizbiyyuun leo. Bali wanasema kuwa ndio maana ya laa ilaaha illa Allaah. Kana kwamba laa ilaaha illa Allaah haina maana nyingine isipokuwa hii. Hawataji ´ibaadah na mengineyo!

al-Haakimiyyah inaingia katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Hakuna kifungu cha al-Haakimiyyah. Ni lazima kuithibitisha Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah kwa aina zake zote. Ama kuchukua tu al-Haakimiyyah na kuacha vipengele vingine, si sawa. Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ndani yake mna ´ibaadah zote na moja wapo ni hukumu kati ya watu na maneno. Hii ni haki ya Allaah (´Azza wa Jalla).

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ

“Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee.” (06:57)

al-Haakimiyyah ni aina miongoni mwa aina ya Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_02.mp3
  • Imechapishwa: 03/07/2018