Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Inahusiana na maudhui ya Salafiyyah Kuwait. Napenda kuweka wazi baadhi ya mambo niliyosikia na niliyoona.

Imaam al-Albaaniy: Ulikuweko kule?

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Mimi nilikuweko Marekani katika kongamano lililokuwa likiendeshwa na QSS. Nilihudhuria kongamano lililopita na nilichoona ni kwamba kama kwamba Shaykh ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq na baadhi ya ndugu huko Kuwait ni wenye kushikamana na mwelekeo huo. Wakati wa kongamano wanadhihirisha Salafiyyah kwa sura ya uvyamavyama na nembo inayokabiliana na nembo ya al-Ikhwaan. Hawaiwakilishi kwa aina ya mfumo kamilifu ambapo lengo lake ni kuwakinaisha wengine ni mamoja watu hao ni Ikhwaaniy, Tabliyghiy au wengineo wenye kukinaishwa nayo. Mwelekeo huu ukiendelea hivo, basi Da´wah itageuka kuwa ya kivyamavyama…

 Imaam al-Albaaniy: Kweli.

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: … na itageuka ni Da´wah ya Ikhwaaniyyah Hizbiyyah ikiwa na sura ya Salafiyyah.

Imaam al-Albaaniy: Mimi huita kuwa ni Ikhwaaniyyah iliyopata chanjo ya Salafiyyah.

Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh: Kitu hichi kinaiharibu Da´wah kikamilifu. Kwa sababu siku miongoni mwa siku kwa mfano Ikhwaaniy, Tabliyghiy au mtu wa kawaida barabarani anaichukia Salafiyyah kwa sababu ya kuchukia ukundikundi huu. Kitu hichi kinaidhuru Da´wah kikamilifu. Mimi mwenyewe nimeona namna baadhi yao hawatendei kazi Sunnah, hawaswali misikitini, hawavai kwa mujibu wa Sunnah na kadhalika. Hii maana yake ni kwamba wameichukulia Salafiyyah kwa muonekano fulani kwa kutaka tu kuitangaza katika nchi fulani, kutaka viti bungeni, wizara na mfano wake.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1003)
  • Imechapishwa: 05/04/2020