Kuna mtu alimwambia Abu Bakr bin ´Ayyaashiy:

“Ee Abu Bakr! Ni nani Suunniy?” Akamjibu kwa jibu zuri na kusema: “Ni yule asiyekasirika pindi kunapotajwa hawaa yoyote.”[1]

Kwa nini? Kwa sababu yeye ni Sunniy ambaye anajinasibisha tu na Sunnah. Haathiriki na Ahl-ul-Ahwaa´ na pindi matamanio yanapopondwa. Haathiri na vitabu vya Ahl-ul-Ahwaa´ na pindi watunzi wao wanapopondwa. Hali hii ni tofauti na mtu ambaye amechafuliwa kwa mambo hayo hata kama atadai kuwa anafuata Sunnah. Pale tu kunapotajwa Bid´ah zake na Bid´ah za kundi lake wamuona akasirika. Mtu asemeje pindi litapohadharishwa moja kwa moja mbele yake? Bila ya shaka huchanganyikiwa.

Ndio maana utaona jinsi baadhi ya Hizbiyyuun wanavyokasirika na sura zao kubadilika pindi tu kunapotajwa makosa ya kundi lao. Kisha baada ya hapo wanajiwa na shaytwaan na anawashawishi kuwa hasira hii ni kwa ajili ya dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ilihali uhalisia wa mambo ni hasira kwa ajili ya pote lake na wafuasi wake, sawa ikiwa atakubali hilo au atakataa. Ni lazima kuyataja makosa na kuyatahadharisha. Utamuona mtu anakasirika kwa ajili ya kutajwa makosa ili yaepukwe, basi utambue kuwa huyo ni mtu wa matamanio na kwenye moyo wake kuna uchafu.

[1]  al-I´tiswaam (1/84) ya ash-Shaatwibiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 09/08/2020