Hivi ndivo wanafunzi watapata heshima

Swali: Umetaja haiba ya heshima ya mwalimu. Lakini baadhi ya waalimu wanafahamu kuwa haiba inapatikana kwa ukali, kichapo na mengineyo. Hivyo wanafunzi wanamuheshimu lakini pamoja na kumchukia na matokeo yake hawachukui elimu kutoka kwake kwa sababu ya kule kumchukia kwao. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Nilisema kuwa mtu anapaswa kujifanyia mwenyewe utu wa kuheshimika, na sio kuwa mkali. Kwa sababu ambaye anataka kuheshimiwa kwa ukali na kichapo hatoheshimiwa. Wakati ambapo wanafunzi watamuona  ameghafilika basi watatumia fursa hiyo kuanza kucheza na kufanya vurugu.

Lakini akionyesha utu kwa njia ya kwamba anawaonyesha wanafunzi kuwa ni mtu siriazi asiyependa mchezo, basi itatosha kule kuwatazama kwa jicho la ghadhabu na kwa mtazamo wa mbali kana kwamba anawakemea kile wanachokifanya. Kwa namna hiyo anakuwa mwenye kuipa nguvu utu wake.

Kuhusu kichapo, kama tunavotambua ni jambo limekatazwa isipokuwa pale kunapokuwa na dharurah. Kichapo hakifanyi mtu kuheshimika. Kinafanya mtu kuogopwa. Hatokuwa mwenye kupendwa na watu. Lakini haiba ya heshima ni kitu kimoja na kuogopwa ni kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49 A)
  • Imechapishwa: 26/05/2021