Swali: Wakati tunapowanasihi watoto na vijana wetu juu ya ISIS wanasema kuwa matendo yao ni Jihaad katika njia ya Allaah. Wanasema kuwa wameona jinsi wamevogawanya “Kitaab-ut-Tawhiyd”, kusimamisha huduud, kuwalazimisha wanawake kuvaa Hijaab na kubomoa makaburi. Vipi tutaraddi utata huu?
Jibu: Utata wa ISIS, na wengine, utaraddiwa kwa kusoma mfumo wake na kama wana mfumo ambao mkusanyiko, Jamaa´ah, ya Waislamu wako nao na hawaendi kinyume nao na wala hawafanyi uasi kwa watawala. Haifai kwa wao kufanya uasi kwa watawala. Wanatakiwa kuwa pamoja na mkusanyiko wa Waislamu; Mkono wa Allaah uko pamoja na mkusanyiko. Wasiunde kundi lililojitenga.
  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu’ http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Muhadharah%20%20-%206%
  • Imechapishwa: 06/11/2016