Hivi ndivo utajua kama ISIS wako katika haki au batili


Swali: Wakati tunapowanasihi watoto na vijana wetu juu ya ISIS wanasema kuwa matendo yao ni Jihaad katika njia ya Allaah. Wanasema kuwa wameona jinsi wamevogawanya “Kitaab-ut-Tawhiyd”, kusimamisha huduud, kuwalazimisha wanawake kuvaa Hijaab na kubomoa makaburi. Vipi tutaraddi utata huu?

Jibu: Utata wa ISIS, na wengine, utaraddiwa kwa kusoma mfumo wake na kama wana mfumo ambao mkusanyiko wa waislamu wako nao na hawaendi kinyume nao na wala hawafanyi uasi kwa watawala. Haifai kwa wao kufanya uasi kwa watawala. Wanatakiwa kuwa pamoja na mkusanyiko wa waislamu; mkono wa Allaah uko pamoja na mkusanyiko. Wasiunde kundi lililojitenga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu'
  • Imechapishwa: 05/09/2020