Hivi ndivo inatukuzwa Qur-aan, na sio kwa kuibusu

Swali: Ni ipi hukumu ya kubusu msahafu? Ni upi usahihi wa yale yaliyopokelewa kutoka kwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) juu ya hilo?

Jibu: Sitambui msingi wa hilo. Imepokelewa kutoka kwa ´Ikrimah – ambaye ni mwanafunzi wa Maswahabah – ya kwamba alikuwa akiubusu na akisema kuwa ni Kitabu cha Mola Wake. Bora mtu asifanye hivo. Kuitukuza Qur-aan kunakuwa kwa kuitendea kazi, kutekeleza hukumu zake, kusadikisha maelezo yake, kuamini zile Aayah zisizokuwa wazi na kutendea kazi hukumu zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 12/11/2021